Saturday, September 19, 2015

CHADEMA Kumshtaki Dr. J.Pombe Magufuli  anayewania Uraisi kwa tiketi ya Chama cha CCM.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepanga kumshitaki mgombea wa urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli kwa madai ya kutumia vibaya nembo za chama hicho.

Ni baada ya Dk. Magufuli kutangaza kuwa nembo ya Movement for Change (M4C) ni  Magufuli  For Change wakati akifanya mkutano wake wa kampeni mkoani Kigoma kwenye Uwanja wa Kawawa uliopo Ujiji.

Katika mkutano huo Dk. Magufuli alisema “hawa jamaa zangu wa Chadema wananipenda, hata ile nembo yao ya M4C ni Magufuli for Change-maana yake Magufuli kwa Mabadiliko.”

Chadema wanaratajia kufungua kesi hiyo Septemba 21 mwaka huu na kwamba, madai hayo yatakwenda sambamba na madai ya kutumia kauli mbiu

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Ngome Kawe, Mwanasheria wa Chadema, John Malya alisema “CCM imekuwa ikivunja sheria za uchaguzi kila siku bila kuchukuliwa hatua yoyote na mamlaka husika, wanatumia nembo za Chadema ambazo zimesajiliwa na kujulikana.”

Hata hivyo imeelezwa, baada ya Dk. Magufuli ‘kuiba’ alama hizo za Chadema; wafuasi wake, bodi ya wadhamini na watu wake wa kampeni walianza kusambaza mitandaoni nembo ya M4C huku wakidai ni nembo mpya ya CCM.

Malya alisema mbali na hilo la kuiba nembo ya chama, wamekuwa na tabia ya ‘kukopi’ na ‘kupesti’ kila hatua inayo pigwa na Chadema na kuzitumia katika kampeni zao.





No comments: