Friday, September 19, 2014

kupigwa kwa wahandishi wa Habari,Dar esalaam,Tanzinia leo


Huyu ni moja kati ya Wahandishi wa habari BADI,kama anavyo honekana akisikitishwa na jambo ambalo limejitokeza leo tar-18/9/2014 kwa kupigwa na kufukuzwa na mbwa wa polisi hapa ktk ofisi za Wizara ya mambo ya ndani Tanzania.

Hali hiilitokea kafra bila kutegemewa Baada ya kuwasili katika ofisi hizo,Mbowe aliitwa na polisi kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusiana na kauli aliyoitoa hivi karibuni ambapo kiongozi huyo alinukuliwa akihamasisha kutakuwa na maandamano ya wafuasi wa chama chake kupinga kuendelea kwa vikao vya bunge maalumu la katiba,
cha kushangaza zaidi hali hii himepingana na kauli ya Makamu wa Raisi Doctor Mohammed Gharib Bilal 
Awali vurugu hizo zilihusisha wafuasi wa Chadema na askari wa kutuliza ghasia FFU, lakini ghafla zikabadilika na kuwa kati ya polisi na waandishi wa habari, 

Kabla ya hapo wabunge kadhaa wa Chadema  walizuiwa na Mahaskari wenye silaha pamoja na Mbwa, kuingia ndani ya ofisi za makao makuu ya polisi
 , akiwemo Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iramba Mashariki Tundu Lissu, Mbunge wa Ubungo John Mnyika na mwenzake wa jimbo la Ilemela Ezekiah Wenje.
Hatua hiyo ilizusha majibizano baina ya pande hizo ambapo wafuasi wa Chadema walikuwa waking'ang'ania wabunge wao waingie ndani kwa madai kuwa baadhi ya wabunge hao wana nyadhifa muhimu ndani ya chama na kwamba ingekuwa vema waingie na kufahamu anachohojiwa Mwenyekiti wao.



                                                                                                                        

No comments: