Dar es Salaam. Kada mpya wa
Chadema, Edward Lowassa jana amerejesha fomu ya kuwania urais,
Waziri mkuu Mstaafu Edward Lowassa akifanikiwa kupata wadhamini milioni 1.6, zaidi ya nusu ya kura za urais ambazo chama hicho kilipata kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.
Waziri mkuu Mstaafu Edward Lowassa akifanikiwa kupata wadhamini milioni 1.6, zaidi ya nusu ya kura za urais ambazo chama hicho kilipata kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.
Naibu
katibu mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu alisema idadi hiyo ya
wadhamini inaashiria ushindi wa kishindo, kwa maelezo kuwa inakaribia
idadi ya kura alizopigiwa katibu mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa
alipogombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Katika
Uchaguzi huo, Dk Slaa alishika nafasi ya pili baada ya kupata kura
2,271,941 sawa na asilimia 26.34, huku Rais Jakaya Kikwete akipata kura
5,276,827 sawa na asilimia 61.17.
Lowassa alipochukua
fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais kwa tiketi ya CCM, kabla ya
kuhamia Chadema, alidhaminiwa na wanachama 870,000 nchi nzima.
Dk
Slaa, ambaye hajaonekana hadharani tangu Lowassa ajiunge Chadema, jana
hakuwapo kwenye ofisi za chama hicho wakati mbunge huyo wa Monduli
alipokuwa akirejesha fomu.
Hakuna kiongozi aliyekuwa tayari kuzungumzia suala lake, lakini baadhi ya maofisa wa Chadema walisema wanaendelea kuchapa kazi.
Kama
ilivyokuwa juzi katika hafla fupi wakati Lowassa akichukua fomu, umati
mkubwa ulifurika na kusababisha Mtaa wa Ufipa uliopo Wilaya ya Kinondoni
kufungwa,
watu walijazana tena na safari hii umati huo ukiwa umebeba mabango ya kumsifu Waziri Mkuu huyo wa zamani.
watu walijazana tena na safari hii umati huo ukiwa umebeba mabango ya kumsifu Waziri Mkuu huyo wa zamani.
Katika
hafla ya jana, makamu mwenyekiti wa Chadema-Bara, Profesa Abdallah
Safari alieleza jinsi Chadema ilivyojipanga kuchukua nchi na siyo
kushinda ubunge na udiwani pekee na kwamba Lowassa amebakiza hatua mbili
tu kuingia Ikulu, jambo walilodai kuwa limeichanganya CCM.
Wakati
Lowassa ambaye alitangaza rasmi kujiondoa CCM na kujiunga na Chadema
Julai 28 mwaka huu akisubiri kupitishwa na Mkutano Mkuu wa chama hicho
utakaofanyika Agosti 4, habari za ndani zinaeleza kuwa vigogo kadhaa wa
CCM watatambulishwa katika mkutano huo.
Habari hizo
zinaeleza watakaotambulishwa siku hiyo ni wenyeviti wa CCM wa mikoa,
wilaya na waliokuwa wabunge wa chama hicho ambao wanamuunga mkono
Lowassa.
Jana Lowassa, aliyekuwa amevaa shati jeupe na
suruali nyeusi na aliyekuwa katika gari aina ya Toyota Land Cruiser VX,
alifika makao makuu ya Chadema saa 9:35 alasiri akiwa pamoja na familia
yake na alipokewa na umati mkubwa wa watu waliokuwa wamebeba mabango
yenye ujumbe mbalimbali.
kama “Chini
ya Lowassa umaskini haupo”, “Kwa Lowassa hata maskini atapata ajira”
na “Kingunge Ngombare-Mwiru karibu Ukawa” . huo ndio Ujumbe wa kwenye mabango yaliyo bebwa na watu
Kingunge ni kada mkongwe wa CCM na anamuunga mkono Lowassa.
na “Kingunge Ngombare-Mwiru karibu Ukawa” . huo ndio Ujumbe wa kwenye mabango yaliyo bebwa na watu
Kingunge ni kada mkongwe wa CCM na anamuunga mkono Lowassa.
Mbali na kubeba mabango,
watu hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kumsifu Lowassa na
kushangilia pale ilipokuwa ikitajwa mikakati ya chama hicho kushika
dola.
Kura milioni 1.6
Akieleza
taratibu na kanuni za kudhamini mgombea urais, mkurugenzi wa
Oganaizesheni na Mafunzo wa chama hicho, Benson Kigaira alisema mgombea
urais anatakiwa kudhaminiwa na wanachama wasiopungua 200.
“Naamini
fomu za Lowassa zitakuwa na idadi hiyo ya wadhamini. Ila baada ya
mgombea kuchukua fomu jioni yake wanachama wa Chadema, wapenzi na
Watanzania walifurika katika ofisi za Kanda, mikoa na majimbo nchi nzima
wakiomba kumdhamini,” alisema Kigaira.
Alisema
wanachama hao walidhani fomu hizo zimepelekwa kila mkoa, kutokana na
kuepuka kuwanyima fursa hiyo chama hicho kilipeleka fomu ili wanachama
wamdhamini na kupewa masharti kuwa lazima wawe wamejiandikisha kupiga
kura, wataje namba zao za simu.
Huku akionyesha fomu
chache za wadhamini kutoka mikoa mbalimbali nchini, Kigaira alitaja
idadi ya watu waliomdhamini Lowassa katika mikoa yote 32 kuwa ni
1,662,397.

No comments:
Post a Comment