Mchungaji Mtikila akichukua fomu ya Uraisi kwa kuzua lingine Tata.
Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila akisaini nyaraka za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) za kuthibitisha kupokea fomu za kugombea Urais zilizokabidhiwa na Ofisa Mwandamizi wa Tume hiyo George Kashura jijini Dar es SalaamMchungaji Mtikila ambaye aliambatana na mgombea mwenza Juma Metu Juma, alitaka ufafanuzi wa kutokuruhusiwa kuwania urais akiwa mgombea binafsi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) imeruhusu.
Mchungaji Mtikila ambaye aliambatana na
mgombea mwenza Juma Metu Juma, alitaka ufafanuzi wa kutokuruhusiwa
kuwania urais akiwa mgombea binafsi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
wakati Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) imeruhusu.
“Siondoki
hapa na wala sitaweza kuchukua hizi fomu hadi mniambie ni wapi nitapata
jibu la tume la kukiuka maagizo ya mahakama ya Afrika.
“Waandishi
embu subirini kwanza mkurugenzi wa uchaguzi aje hapa ilia atoe
ufafanuzi na nyie msikilize mkaandike ukweli kwa sababu hii siyo haki ni
sawa na kudharau mahakama,” alisema.
Baada ya kuzozana
na maofisa waliokuwa wakimkabidhi fomu hizo, walilazimika kumuita
mkurugenzi wa uchaguzi Kailima Ramadhani, ambaye alimwambia kwamba
sheria hairuhusu.
“Sisi tunafuata sheria mwenyekiti
kama hicho kipengele kingekuwapo tungekuruhusu uchukue fomu hizo, lakini
hapa tunabanwa na sheria tunaruhusu kutoa fomu kwa watu wanaotoka
kwenye vyama vyao,” alisema Ramadhani.

No comments:
Post a Comment